Wanawake mkijiuliza mambo haya kamwe hamtawalaumu wanaume
Ukweli ni kuwa wanajihangaisha bure iwe kwakujua au la.
Wanawake wapo kwaajili ya wanaume, hili kila mmoja hulifahamu. Hivyo kitendo cha mwanaume kumiliki wanawake zaidi ya mmoja ni ishu inayoongozwa na nature tuu.
Hakuna mwanamke anayeweza kuwa na wanaume wengi na ikiwa yupo basi mawazo yake huongozwa na shida mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kiulinzi, n.k.
Lakini wanawake wanaojiweza au waliowezeshwa hawawazi kumilikiwa na Mwanaume zaidi ya mmoja. Hili ni tofauti kwa sisi jinsia ya kiume. Mwanaume hata awe na Mke au mpenzi mzuri bado atajikuta anataka kama sio kutamani wengine zaidi. Hiyo ni silika ya kiume.
Wanawake hawapaswi kuwalaumu wanaume kwa tabia za kutamani tamani wanawake wengine bali hupaswa kuhakikisha mume wake anajizatiti naye mpaka hakosi pakutokea. Wanawake wengi wamekuwa wanafalsa ya uongo kuwa eti mwanaume halindwi au hachungwi. Na wengi wanaosema hivi huwa na dalili za kukata tamaa kama sio uzembe na kupuuzia mambo.
Wanawake wangejiuliza yafuatayo wala wasingethubutu kulaumu wanaume:
1. Kwa nini wanaume wanahisia za karibu na huwahi kukinahi mapema kuliko wanawake?
2. Kwa nini mwanamke anaukomo wa kuzalisha mbegu za kike afikapo umri Fulani tofauti na mwanume ambaye huzalisha hata afikishe miaka 400?
3. Kwa nini mwanamke huruhusu yai moja kila mwezi ambalo ndilo hufanyiwa Fertilization?
4. Kwa nini wanawake wawe wengi kuliko wanaume?
5. Kwa nini mwanamke awe na bikira ikiwa ni Alama ya kutokuguswa kwake wakati wanaume hawana?
6. Kwa nini wanawake wanakua haraka tofauti ya wanaume?
ikiwa maswali hayo wanawake wangejiuliza basi kusingekuwa na malalamiko kuhusu wanaume kuwa na tamaa.
Angalizo:
Hata ukiwa Mwanaume Sheria za Mungu hazivunjwi kwa kigezo chochote.