Orodha ya vitabu alivyosoma Zitto Kabwe mwaka 2016,Zitto amevitaja vitabu vyote na sababu za yeye kusoma vitabu hivyo.



Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto amevitaja vitabu vyote na sababu za yeye kusoma vitabu hivyo pamoja na kile alichojifunza kwenye kila kitabu.

“Mwaka 2016 nimesoma vitabu 53. Nimeongeza vitabu nilivyosoma tofauti na mwaka 2015 lakini sikuweza kufikia idadi ya mwaka 2014 ambapo nilisoma vitabu 56. Hiyo ndio rekodi ya juu zaidi tangu nilipoanza kuorodhesha vitabu nilivyosoma mnamo mwaka 2012. Mwaka 2013 niliorodhesha vitabu vichache zaidi nilivyosoma.

Mafanikio makubwa ya mwaka huu ni kuongeza vitabu vya Riwaya (fiction), ingawa mtaona mwandishi mmoja, Jeffrey Archer amejitokeza sana kuliko wengine. Hiyo ni kutokana na kusoma kazi yake moja nzuri na yenye mafunzo mengi sana kwa wanasiasa iitwayo First Among Equals.

Kazi hiyo ilinifungua macho na kuanza kusoma Clifton Chronicles (vitabu 7) na kufuatia mapendekezo ya wanaonifuata kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram niliweza kupata vitabu vingine vya mwandishi huyu. Kwangu mimi Bwana Jeffrey Archer ni Mwandishi wa Riwaya Bora wa Mwaka 2016.

Licha kutaka kuanza na Gavana Ben Bernanke, nilijikuta naanza na vitabu kuhusu Russia na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin. Msukumo huo ulitokana na namna nilivyomsoma Mtawala mpya wa Tanzania Rais John Magufuli kulinganisha na Kiongozi wa zamani wa nchi yetu Rais Jakaya Kikwete.

Kitabu nilichoanza nacho mwaka 2016 ni The Strongman: Vladimir Putin and the Struggle for Russia kilichoandikwa na Angus Roxburgh. Baada ya kusoma kitabu hiki nilijikuta ninanunua vitabu vingi kuhusu Urusi, Putin, Udikteta, Demokrasia na Maendeleo ili kuweza kuelewa mwelekeo wa Siasa za Tanzania za sasa.

Vitabu hivyo vimenisaidia sana kujua namna ya kutafsiri watawala wapya kiasi cha kuunda neno Dikteta Mamboleo (neo-dictatorship) na kuipa tafsiri yake mnamo tarehe 29 Septemba 2016; kwamba Dikteta Mamboleo ni mtawala ambaye ana uzalendo usio tiliwa shaka na anahangaika kuleta maendeleo ya nchi yake lakini hataki kuhojiwa kwa namna yeyote ile.

Mwaka 2016 pia ulinifunua kuhusu uwezo mkubwa na umahiri wa wachapishaji wa Vitabu wa ndani. Nilipata fursa adhimu ya kuzungumza na Mzee Walter Bgoya wa Mkuki na Nyota Publishers. Vitabu kadhaa nilivyosoma katika orodha ya mwaka huu vimechapishwa na Mkuki na Nyota. Nilijifunza mengi mapya ya historia ya nchi yetu na Afrika nzima. Juzuu za masimulizi ya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika nilizipata kutoka Mkuki na Nyota na humo nilipata mambo mapya mengi sana.

Kisa kimoja kinachonichekesha kila nikumbukapo ni hadithi ya Rais Khama (baba) wa Botswana alivyobeba machungwa kwenye ndege kumletea zawadi Mwalimu Nyerere akimtania kuwa sera zake za Ujamaa zilileta njaa nchini.

Mwaka huu ninawawekea mapema vitabu nilivyosoma tofauti na miaka iliyopita kwa sababu kwa uwezo wake Manani sitaweza kusoma vitabu vingine baada ya leo kwani nitakuwa na majukumu ya malezi.
Karibu kwenye orodha ya vitabu vyangu mwaka 2016
1. The Strongman: Vladimir Putin and struggle for Russia – Augus Roxburgh
2. Putin’s Progress – Peter Truscott
3. The Putin Mystique: Inside Russia’s Power Cult – Anna Arutunyan
4. The Invention of Russia: The Journey from Gorbachev’s Freedom to Putin’s War – Arkady Ostrovsky
5. I am going to Ruin Their Lives: Inside Putin’s War on Russian Opposition – Marc Bennet
6. Red Notice: How I became Putin’s no 1 enemy: Bill Browell
7. Ruling Russia: Authoritarianism from the Revolution to Putin – William Zimmerman
8. Dictator’s Learning Curve: Inside the global debate for Democracy – William Dobson
9. Dictator’s Handbook: Why bad behavior is almost good politics – Bruce Buener de Mesquita and Alastair Smith
10. Dictator – Tom Cain
11. The Warlord- James Steel
12. Tanzania: A Political Economy ( 2nd Ed ) – Andrew Coulson
13. Thieves of the State: Why corruption threatens global security – Sarah Chayes
14. How to Run A Country – Marcus Tullius Cicero
15. The End of Karma: Hope and fury among India’s young – Somini Sengupta
16. The Hidden Wealth of Nations: The scourge of tax havens – Gabriel Zucman
17. Mystery of Capital – Hernando De Soto
18. So long a letter – Mariama Ba ( Special thanks to January Makamba for recommending this to Bunge Readers’ Club )
19. The Fifth Mountain – Paulo Coelho
20. First Among Equals – J. Archer
21. Kane and Abel – J. Archer
22. Best Kept Secret – J. Archer
23. The Sins of the Father – J. Archer
24. Only Time Will Tell – J. Archer
25. Shall we Tell the President – J. Archer
26. Mightier Than The Sword – J. Archer
27. The Fourth Estate – J. Archer
28. Honour Among Thieves – J. Archer
29. Cometh The Hour – J. Archer
30. This was a Man – J. Archer
31. The New Collected Short Stories – J. Archer
32. Building a Peaceful Nation – Bjerk
33. Burundi Peace Dialogue- Pierre Buyoya
34. Burundi: The Biography of a small African Nation – Nigel Weltt
35. The Thabo Mbeki I know – ed. Sifiso Mxolisi and Miranda Staydom (Special Thanks to Amb. Ami Mpungwe, a contributor to the very book)
36. Clinton Cash – Peter Schweizer
37. Connectography: Mapping the Global Network Revolution – Parag Khanna
38. The Rohingyas: Inside Myanmar’s Hidden Genocide – Azeem Ibrahim
39. Stringer: A Reporter’s Journey in the Congo – Anjan Sundaram
40. Uchambuzi wa Sera, Uongozi na Maslahi ya Watanzania – CSL Chachage
41. Haki, Amani na Maendeleo: Nafasi na Wajibu wa Mahakama Tanzania – S J Bwana
42. Wanawake wa TANU – Susan Geiger (a special thanks to my wife for bringing this home)
43. African Socialism or Socialist Africa – A M Babu ( Special Thanks to Dr. Khamis Kigwangalla for suggesting it to Bunge Readers Club and Ezekiel Kamwaga who lent it to me )
44. The Courage to Act – Ben Bernanke
45. The Litigators – John Grisham
46. White Lioness – Henning Mankell
47. The Dogs of Riga – H. Mankell
48. Fifth Woman – H. Mankell
49. Kennedy’s Brain – H. Mankell
50. Treachorous Paradise – H. Mankell
51. Harusi ya Dogoli – Athumani Mauya
52. Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere – Peter Bwimbo
53. The Hashim Mbita Project: Southern African Liberation Struggles Contemporaneous documents ( 1960 – 1994 Volumes 1, 3, 5, 6 & 7 ) – Ed. A J Temu and J N Tembe