Simba ya rejea kileleni baada ya kuifumua Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara


Magoli ya Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim yameirejesha tena Simba katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Mzamiru alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 64 kabla ya Mohamed Ibrahim ‘MO’ kuihakikishia Simba ushindi na kuendeleza ubabe dhidi ya Ndanda FC.

Simba imerejea kwenye nafasi yake baada ya jana (Jumamosi December 17) Yanga kushinda mchezo wake dhidi ya JKT Ruvu na kukaa kileleni mwa VPL kwa muda ikisubiri matokeo ya Ndanda vs Simba.

Ushindi wa Simba unaifanya kufikisha pointi 38, pointi mbili mbele ya Yanga huku timu zote zikiwa zimecheza mechi sawa hadi sasa (16).