Yanga yapaa hadi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, Yatoa kipigo kizito kwa JKT RUVU
Yanga imepaa hadi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Ushindi dhidi ya JKT Ruvu unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 pointi moja mbele ya mahasimu wao Simba ambao watacheza kesho dhidi ya Ndanda FC mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili ya VPL.
Deusi Kaseke alifunga goli la kwanza la Yanga dakika ya 37 kipindi cha kwanza kwa kuunganisha pasi ya Simon Msuva
Msuva akafunga bao la pili dakika ya 57 kabla ya kufunga tena dakika ya 90 na kuilaza JKT Ruvu huku Yanga ikikaa kileleni mwa ligi ikisubiri matokeo ya Simba.
Msuva alikuwa kwenye ubora wake kwenye mchezo dhidi ya maafande wa JKT Ruvu na hiyo inatokana na kufunga magoli mawili na ku-assist bao moja ambalo lilifungwa na Kaseke.