Achomwa moto kwa tuhuma za wizi wa kuku
Mkazi wa Kijiji cha Busagami wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, Leonard Mugusa ameuawa na mwili wake kuchomwa moto akituhumiwa kwa wizi wa kuku.Mugusa maarufu kwa jina la Kakono alizingirwa na kushambuliwa kwa silaha za jadi na kundi la watu juzi alfajiri baada ya kukutwa na kuku watano, mali ya Richard Mkungu, pia mkazi wa kijiji hicho.Mashuhuda wa tukio walisema kauli za vitisho alizotoa Mugusa, akiahidi baada ya kurudi kama angepelekwa polisi, angewashughulikia wote waliohusika, ndio zilisababisha wapandwe na hasira na kumshambulia na kuchoma moto mwili wake.Diwani wa Kata ya Namilembe, Innocent Josephat n alisema amesikitishwa na tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha kujichukua sheria mkono.