Balaa kubwa Amuua Mkewe Kisa Tsh 200 tu...!!!
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, dada wa marehemu, Siwema Masoud alidai kuwa awali ndugu yake huyo alimpigia simu kuwa Januari 19 usiku alipigwa na mumewe kwa kupotea Sh 200.
Alisema siku moja kabla alimpa mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka mitano Sh 200 akanunue maandazi, lakini mtoto huyo aliporwa fedha hiyo na wenzake, akashindwa kurudi nyumbani kwa siku mbili, akarudi siku ya ugomvi wa wawili hao na mumewe kukasirika.
Alidai kuwa mume huyo, Kunduwenda Kiza (37) akimfokea mtoto huvyo mama mtu kuamua kumwomba radhi mumewe huyo lakini bila mafanikio kwani katika hali ya kushangaza mumewe alimpiga mpaka kupoteza fahamu.
Siwema asilimulia kuwa kesho yake saa 9.45 alfajiri hali ya Zubeda ilibadilika na kutokwa damu sehemu mbalimbali zilizo wazi mwilini mwake, mumewe akamkimbiza kwenye zahanati ya kijiji hicho na Januari 20, alipewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa ya Maweni.
Alisema Januari 21, saa 12.45 Zubeda alipoteza maisha hali iliyowapa mashaka na kufikisha taarifa Polisi kwa uchunguzi maiti lakini walipokwenda na askari hospitalini wakaambiwa jalada halionekani.
Hata hivyo, mganga aliyetambuliwa kwa jina la Dk Muganyizi alijitolea na kuufanyia uchunguzi mwili huo na baada ya uchunguzi maiti alibaki mochari.
Lakini wakati ndugu wakijiandaa kwenda kuchukua mwili walishangaa kukuta umeondolewa, na kwa msaada wa polisi waliukamata ukisubiri kusafirishwa kinyemela.
Mwandishi alifika Maweni na kugundua kuwa kabla ya kifo alilazwa wodi 2(b) ya wanawake huku jalada lenye taarifa zake likiwa limetoweka huku uchunguzi wa Mganga ukibaini kuwa na majeraha ndani ya mwili yaliyosababisha kuvuja damu kulikochangia kifo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ferdinand Mtui alikiri kupokea taarifa za kifo cha kutatanisha cha Zubeda.
Kamanda Mtui alisisitiza kuwa mshukiwa Kiza anashikiliwa na Polisi kwa upepelezi na ikibainika ametenda kosa hilo, atafikishwa mahakamani.