Demu wa Kalala Junior Akumbwa na Sekeseke la Fumanizi Live
Mwigizaji wa Bongo Movies, Mumy Mushi ambaye miezi kadhaa iliyopita aliripotiwa kuwa kwenye uhusiano matata wa kimapenzi na mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Hamza ‘Kalala Junior’ amekumbwa na sekeseke baada ya kufumaniwa laivu akiwa chumbani na mume wa mtoto wa kigogo ambaye kwa sasa ni marehemu (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum).
Tukio hilo lililofunga mtaa lilijiri kwenye hoteli moja maarufu iliyopo maeneo ya Sinza-Kijiweni, Dar baada ya mwigizaji huyo na mume wa mtoto huyo kigogo ambaye pia ni msanii aliyejulikana kwa jina moja la Dennis kuwepo katika hoteli hiyo kwa muda mrefu kwa madai kuwa wapo kambini. Shuhuda wetu aliyekuwepo eneo la tukio alilithibitishia Wikienda kuwa, Mumy alianza uhusiano na mume huyo wa mtu miezi kadhaa iliyopita wakati wakirekodi sinema bila mkewe kushtukia.
Mpashaji wetu huyo alifunguka kuwa, kuna baadhi ya marafiki wa wanandoa hao walimtonya mke huyo kuhusu Dennis kuwa na mchepuko na kupewa maelekezo hadi sehemu walipokuwa wakijiachia na ndipo alipoandaa kikosi kazi na kwenda kuwafungia kazi usiku mnene. “Unajua mke wa jamaa ni mpole hivyo alivyoambiwa alianza kuwafuatilia na kugundua hadi sehemu walipo hivyo kuamua kuwavamia,” kilisema chanzo hicho. Chanzo chetu kilizidi kutiririka kuwa, Mamy na Dennis
walikuwa ndani ya hoteli hiyo kwenye chumba namba 8, wakiwa wamejisahau ndipo mke huyo na ‘jeshi’ lake alipovamia chumbani hapo na kumkuta mumewe na Mamy wakifanya yao.
“Kiukweli mwanaume alivyokutwa hakuwa na jinsi zaidi ya kutoka chumbani hapo na kwenda moja kwa moja kwenye gari lake huku mkewe akipachimba na Mamy kabla ya kushikwa asianguke kutokana na tatizo la presha alilonalo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Wikienda liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Mamy ambaye aliposomewa shitaka lake alisema kuwa anachojua Dennis alishaachana na mkewe na ndiyo maana alikuwa naye na yeye sasa hivi ni mjamzito.
“Yeye ndiye aliniambia kuwa wameshaachana na mkewe ndiyo maana mimi nikawa naye na hata huyo mwanamke alivyokuja kufumania nilijua wazi walishaachana lakini alitaka tu kunifanyia fujo na kunidhalilisha,” alisema Mamy.
Kwa upande wa Dennis ambaye mkewe alimfumania na Mamy alisema yeye kama mwanaume aliteleza lakini alijirudi na ameshamuomba msamaha mkewe na wala hana mpango na Mamy. “Jamani najua nilikosea, nikateleza, lakini kiukweli ninamheshimu mke wangu na ataendelea kuwa mke wangu siku zote,” alisema Dennis.
Gazeti hili lilipompa nafasi mtoto wa kigogo huyo aliyemfumania mumewe alisema kuwa ameshamsamehe Dennis na amempa nafasi nyingine na maisha yao yanaendelea. “Tangu mwaka huu umeanza hali ya ndoa yangu ilikuwa mbaya sana lakini sasa niko sawa na mume wangu,” alisema mke huyo.