Jacqueline Wolper Apigilia Msumari ishu ya Kumpiga chini Harmonize
Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai kwa sasa anauguza majareha ya moyo aliyoyapata kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Harmonize.
Wiki moja iliyopita muigizaji huyo aliweka wazi kuwa hayupo tena kwenye mahusiano na muimbaji huyo wa wimbo ‘Matatizo’ kauli ambayo ilileta ukakakasi cha mashabiki wakidhani huwenda ikawa ni kiki.
Jumamosii hii malkia huyo wa filamu alirudi tena na kuweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano Harmonize na kudai habari zinazoendelea katika mitandao kwamba wapo pamoja sio za kweli.
“Kuna watu wengi napokea simu zao na wengine mmekuja hadi dukani kuniuliza kama mnayoona niya kweli au lah wengi nimewaambia sina la kusema ila baada ya kutafakari nimeona bora niwaambie upande wangu. Since i’m young yaani hata ukiuliza wanaonizunguka watakuambia mi napenda mapenzi, na naheshimu sana mahuasiano. Yaani kutoka rohoni usanii pembeni as a person mimi Jacky ukiniona niko na mtu na nimemuweka hadi public basi ujue nina mapenzi nae kingine nina moyo wa nyama ninayo ambayo naweza kubeba kifuani mengine siwezi kuumizwa moja wapo,” aliandika Wolper Instagram.
Aliongeza, “Yaani nawaapia mimi kitu kidogo naweza kikanikaba rohoni nikawa naumia muda wote. Halafu ikishakuja kwenye maumivu siwezagi tena drama, naongeaga ukweli hata uwe wa aina gani, mashabiki zangu nyie mashahidi ninaelezeaha story nzima pasipo kuficha japo yaweza kuwa na aibu ama vitu nilivyokua navumilia yakinishinda naongeaga. Kwa sasa hivi naugulia moyoni. Hizi drama na story za kutunga zinazoendelea please please.. naomba! Heshimuni feelings zangu na mimi nina moyo, naombeni nideal na hili personal kwanza nikiweza kulimeza nitawashirikisha. Hayo mengine mnayosIkia nawahakikishia ni drama tu na kiki ambazo watu wanajitengenezea story wapate listeners, followers na likes,”.