MJUE MNYAMA TEMBO NA SIFA ZAKE

TEMBO NI NANI ?
kwa wanaomfahamu au kutokumfahamu,tembo ni mnyama mkubwa kuliko wote duniani aishie nchi kavu.
Bila ya kusahau kuwa nyangumi ndie mnyama mkubwa kuliko wote hali ya kuwa wao wanaishi baharini.

AINA ZA TEMBO (species).
duniani tuna aina kuu mbili za tembo.
>african elephant.
>asian elephant.
Tembo wa asia (ASIAN ELEPHANT) tembo anaeweza kufugika,ni tembo mwenye ukaribu kabisa na binadamu na zamani alitumika pia katika masuala ya vita.

Huyu ni tembo mwenye pembe (tusk)nyepesi zaidi kuliko ya tembo wa afrika.
Tembo wa afrika na mkubwa zaidi na mkali kuliko wa asia.
Kawaida tembo wa afrika wanatabia ya kulipiza visasi (VIGAROUS ATTACK) hivyo kuwa katika mnyama wa kundi la BIG FIVE.

PEMBE ZAKE (TUSK).
pembe zake humsaidi katika mambo mengi kama wakati wa kupigana pia wakati wa kuchimba chini kutafuta maji au chumvi.
Pembe hizo ndio chanzo cha majangili wengi kuwaua.
Pembe hizo pia hutumika katika kubandualia magome ya miti hata kuangusha miti pia.

MKONGA WAKE (TRUNK).
Kwanza kwa kifupi,NI PUA NDEFU ILOYOREFUKA mdomo wa tembo upo chini ya mkonga huo.
Mkonga hutumika katika kukatia nyasi wakati akila na kufutia maji wakati wa kunywa.
Kwa kuwa mkonga ni pua ndefu,wakati wakipata tiba madaktari wanapaswa kuwa makini ili tembe asije kulali mkonga wake na hivyo huweza kusababisha kifo kwa kukosa hewa.

Kundi la tembo huongozwa na tembo jike aitwae MATRIARCHY.
Mkonga hutumika pia katika mawasiliano yao kama wanyama.

MIMBA.
Tembo ni mnyama mwenye kubeba mimba kwa muda mrefu zaidi.
Hubeba mimba kwa miezi 18 hadi 22 sawa na miaka miaka miwili.

UJANGILI.
=tembo hufanyiwa ujangili sana huku ujangili mkuu ukiwa ni wa kusaka pembe zake.
Jumuia za kimataifa na taifa kiujumla zinapaswa kusimama ili kulinda maisha ya wanyama hawa na vizazi vyao.
Ujangili wa tembo ni hasara kwa taifa.