Mtoto wa Mbunge Anaswa Usiku na Golikipa Timu ya Mtibwa Sugar
Dar es Salaam: Binti wa aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM), Naima Shaa amezua balaa kwa mara nyingine baada ya kunaswa akijiachia kwa mapozi ‘tata’ na golikipa namba moja wa Timu ya Mtibwa Sugar, Saidi Mohamed ‘Nduda’.
Tukio hilo lililoacha gumzo kwa muda lilijiri katika Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama, Dar ambapo wawili hao walikuwa wamekwenda kustarehe.
Kwa kamera ya shushushu wetu, Nduda alifika ukumbini hapo akiwa na washkaji zake na Naima naye alikuwa kivyake lakini walipokutana hali ilibadilika na kuanza kufanya yao.
“Walionesha kama watu waliomisiana kitambo. Nduda alipomuona Naima tu, alimfuata harakaharaka na kuanza kupiga naye mapicha tata kabla ya kukumbatiana na kuzungumza kwa muda huku wengine wakisema kuwa ni mrithi wa aliyekuwa mpenzi wa mwanadada huyo ambaye ni kipa wa Simba, Peter Manyika Jr,” alifunguka shushushu wetu na kuongeza: