Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora yahamia Dodoma rasmi leo
Waziri wa utumishi wa umma na utawala bora Angela Kairuki leo January 23 2017 ameiaga rasmi Dar es salaam na sasa ofisi za Wizara hiyo zinahamia Dodoma katika ofisi mpya ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais, agizo ambalo linawataka ifikapo February 28 2017 ofisi za serikali ziwe zimehamia Dodoma.
Nje ya Wizara hiyo Wafanyakazi walionekana wakipunga mikono kwa ishara ya kuaga ambapo Malori ya Jeshi ndio yanayotumika kuhamisha mizigo ambapo Waziri Angela Kairuki ameeleza kuwa vifaa hivyo ni vya kundi la kwanza linalohusisha Uongozi wa juu wa Wizara.
Vifaa hivyo vya ofisi vilivyosafirishwa kwa awamu ya kwanza ni vya Waziri wa nchi ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, katibu mkuu na naibu katibu mkuu na baadhi ya wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi, maafisa waandamizina watumishi wengine na kwamba jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza……… unaweza kuitazama hii video hapa chini kujionea