Waziri Nchemba asema"Hatutamhukumu mtu kwa kazi anayoifanya, tutamhukumu kwa kosa analolifanya"
Polisi mkoani Morogoro mpaka sasa inawashikilia watu 24 kwa mahojiano zaidi kuhusu tukio hilo. Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza nguvu zaidi ya dola iongozwe katika maeneo hayo mpaka mhusika wa tukio hilo atakapopatikana.
Hili ni tukio la pili tangu Waziri Mwigulu awepo mkoani Morogoro la kwanza likiwa la Fabiano Bago mkazi wa kolelo wilaya ya Morogoro ambaye alijeruhiwa maeneo ya kichwani kwa sime na watu wa jamii ya kifugaji mara baada ya kumuona akiongea na simu wakidhani anawataarifu polisi na Fabian alifariki dunia kutokana na majeraha aliyopata