UEFA ligi Uchambuzi na Dondoo za kubeti, Mechi zote za leo



Arsenal itaikabili PSG, Barcelona dhidi ya Celtic, Monchengladbach dhidi ya Manchester City soma kupata dondoo za kubeti



Arsenal vs PSG
: Utabiri

Itakuwa mechi ngumu katika uwanja wa Emirates Arsenal watakapowakaribisha Mabingwa wa Ufaransa PSG Jumatano usiku. Yeyote atakayeshinda kati ya timu hizo mbili atakaa kileleni mwa kundi A Ligi ya Mabingwa.

Arsenal kwa sasa ndiye kinara wa kundi hilo kwa tofauti ya magoli na hawajapoteza mechi katika hatua hii msimu huu. Timu zote mbili zina pointi 10 na zimeshinda mechi tatu, moja zilisare katika mechi ya kwanza zilipokutana Ufaransa. Hata hivyo sare katika mechi hii itaiweka Arsenal kieleni bado.

Rekodi za Arsene Wenger na Arsenal dhidi ya miamba wa Ufaransa zinabeba uzito mkubwa, na zitaamua mchezo. Kwa hakika mechi itakuwa ngumu kulingana na uwezo wa timu hizo mbili. Arsenal hawajafungwa katika mechi 16 kwenye michuano yote, wakati PSG wakiwa hawajapoteza mechi 10 za mwisho katika michuano yote.

Kuna uwezekano mkubwa mechi ikaishia sare kama ilivyokuwa mechi ya kwanza; utabiri wetu ni 1-1.

Celtic vs Barcelona: Utabiri

Hakuna shaka kwamba Celtic ni timu nzuri inapokuwa nyumbani, lakini bado si timu iliyo thabiti. Jambo moja tunaloweza kusema ni kwamba hawatachezea kipigo kizito dhidi ya miamba wa Barcelona nyumbani, mbele ya mashabiki wao. Wamefungwa mara mbili na kushinda mara moja katika mechi zao tatu za mwisho nyumbani dhidi ya Barcelona.

Tukizingatia hali ya majeruhi Barcelona Celtic wana uwezo wa kuzishangaza timu kubwa, timu ya nyumbani inaweza kushinda 2 au zaidi.

Atletico Madrid vs PSV
: Utabiri

Katika viashiria vyote, Atletico Madrid tayari wameshafuzu kucheza hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa. Wamedhamiria kumaliza kileleni mwa kundi watakapoikaribisha PSV katika dimba la Vicente Calderon Jumatano usiku.

Ndio vinara wa kundi D wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 4. Watakuwa vinara wa kundi D iwapo watashinda na Bayern itatoa sare au Bayern ifungwe alafu washinde.

Licha ya matokeo dhaifu ya Atletico Madrid wiki za hivi karibuni, bado wanapewa nafasi kubwa kushinda mechi hii. Vijana wa Simeone watajituma kwa nguvu zote kujihakikishia ushindi mnono. Rekodi mbovu ya PSV dhidi ya timu za Hispania huenda bado ikaendelea kuwasumbua na mechi itakuwa ngumu kwao.

Monchengladbach vs Manchester City
: Utabiri

Borussia Monchengladbach walinyukwa 4-0 na Manchester City timu hizo zilipokutana kwenye mechi ya kwanza ya michuano hiyo katika uwanja wa Etihad. Miamba hao wa Borussia walikwenda kupoteza kwa kichapo cha 2-1 nyumbani dhidi ya Barcelona kabla ya kuanza kupata pointi. Waliifunga Celtic mjini Glasgow kwa ushindi wa 2-0 na kujipatia ushindi wa kwanza, lakini walishikiliwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya timu hiyo katika mechi ya marudiano.

Klabu hiyo ya Bundesliga haipo katika hali nzuri na wameshindwa kupata ushindi katika mechi nne za mwisho katika michuano yote, ambapo mechi 2 za mwisho walifungwa. Manchester City kwa upande mwingine imekuwa na mwenendo mzuri wa ushindi katika mechi zao za mwisho.