Huddah Akiri Kufanya mapenzi na Wizkid,...!!!
MODO na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa Season 8, Huddah Monroe ameweka wazi kuwa alishawahi kubanjuka kimapenzi na staa wa muziki kutoka Nigeria, Ayo Balogun ‘Wizkid’.
Huddah aliyasema hayo baada ya kuachia kipande cha video katika mitandao ya kijamii kikimuonesha akiimba moja ya nyimbo za Wizkid na kusema kuwa amekuwa ni mwanamuziki wake wa muda wote;
“Mungu mjalie maisha marefu Wizkid kwa sababu siwezi ishi bila muziki wake. Nimekuwa nikisikiliza kila wimbo wake. Wizkid amenipa kila hali ya kujisikia raha.”
Baada ya kuandika hivyo, wapo walioungana naye na wengine wakamshambulia kuwa anajigonga kwa Wizkid ampende ndipo povu lilipoanza kumtoka;
“Hata mkisema vipi tayari nimeshabanjuka naye. Hata ninachoongea kuhusu muziki ni kweli yupo juu.”