Msanii kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond ‘Rayvany akana kumtundika Mimba Faima Ila........
Msanii kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond ‘Rayvany’ amekuwa akitajwa kutoka kimapenzi na modo wao anayefahamika kwa jina la Faima na taarifa zikavuja kuwa ‘mtoto’ huyo mzuri sasa ana ‘kibendi’ chake.
Ikadaiwa na chanzo kilicho karibu na wawili hao kuwa, uhusiano wao umekuwa wa siri sana na wa muda mrefu licha ya wakati mwingine kushindwa kujizuia kuanika hisia zao mtandaoni.
Kufuatia madai hayo, Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Rayvany ili kuweka wazi ishu ya kumpa mimba Faima ambapo alifunguka: “Kwanza mimi sina uhusiano na Faima na sijampachika mimba kama wanavyosema ila yeye ni mtu wangu wa karibu sana. Yale ninayofanya kule mtandaoni, nafanya kama mshikaji wangu.”
Hata hivyo, licha ya yeye kukana kuwa na uhusiano naye, Ijumaa lilimtafuta Faima kupitia simu yake kuzungumzia madai ya kuwa mjamzito bila mafanikio lakini aliwahi kukiri kuwa Rayvany ni baby wake na wala hawezi kuficha.