KIMENUKA TENA!!!!!!Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ametaja majina mengine 65 ya watu wanaotakiwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya akiwemo Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, mchungaji Gwajima na Mbunge wa zaman Idd AZAN.
Hii ni awamu ya pili baada ya awali kukamatwa watu 112 ambao baadhi wameachiwa kwa dhamana pamoja na kupewa masharti ya kuripoti mahakamani mara mbili kwa mwezi.
Watajwa wote wa awamu hii ya pili amewataka kufika kituo cha Polisi cha kati siku ya Ijumaa.