Showing posts with label Afya. Show all posts

Faida ya Ukwaju kiafya mwilini



UKWAJU ni tunda lenye faida nyingi mwilini mwa mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa kwa mwanadamu

Ukwaju unapatikana kwa wingi sana sokoni. Unaweza kutengeneza juisi kwa kuandaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni, uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu.

Ipua uache kwa muda upoe, andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juisi yako kwa uangalifu, weka sukari kwa kiasi unachopendelea (kama una kisukari weka asali) pia ili kupunguza ukali

unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata ladha, weka kwenye friji na acha ipoe, tayari kwa kunywa.

Kuna faida kubwa ya juisi kwani ni chanzo kizuri cha viua sumu mwilini ‘antioxidants’ ambavyo huzuia saratani (cancer), una Vitamini B na C vilevile “carotentes,” hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo.

Ukwaju huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni, husaidia myeyusho na mmeng’enyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa.

Ukwaju husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders), kurahisisha choo (laxative), husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo, husaidia ngozi kuwa nyororo, vilevile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda, pia husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo).

Read More »

Mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya yaongoza kwa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Tanzania

Kutokana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kupungua kwa asilimia 50 duniani kote na kupelekea watu milioni 2.1 tu kuambukizwa Virusi vya Ukimwi katika mwaka 2015,kumeibua matumaini mapya ya kuwa na watu wasio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko aliwaambia waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam kuwa, nchini Tanzania maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nayo yameshuka kwa asilimia 20 ambapo watu 54,000 wameambukizwa virusi hivyo kwa mwaka 2015 pekee.

Dkt. Maboko alisema, Ukimwi bado ni janga kubwa duniani na taifa kwa ujumla huku akitaja kundi la wanawake kuwa ndilo lina kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU huku mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya ukiwa na kiwango cha juu cha maambukizi hayo kitaifa.
Aidha, alisema serikali imejiwekea mikakati kuhakikisha kuwa waliogundulika kuwa wameathirika wanaanzishiwa dawa, kuhimiza matumizi ya mpira wa kiume, kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 29 na kutoa elimu kwa wanawake wanaojihusisha na ngono, kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Read More »

Serikali yatoa taarifa ya Gharama Za Matibabu Ya Dawa Ya Sumu Ya Nyoka Nchini

Kama tunavyofahamu, nchi yetu ina aina mbalimbali za nyoka ambao pindi wakimuuma mtu huleta madhara mbalimbali ya kiafya. Aidha tunafahamu kwamba tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwezo wa wananchi kumudu gharama za matibabu ni mdogo.


Dawa za kutibu sumu ya nyoka huagizwa kutoka nje ya nchi. Dawa hizo siyo tu hazipatikani kwa urahisi, bali pia zinapatikana kwa gharama kubwa. Bei ya kununulia dawa hizi ni kati ya dola za kimarekani 55 hadi 85 (yaani shilingi za kiTanzania 118,250 hadi 182,750) kwa kichupa kidogo (vial) kimoja. Kichupa hicho huweza kutumika kwa wagonjwa wanne, lakini mara tu baada ya kufunguliwa dawa hiyo huwa haifai tena kutumika ndani ya mwezi mmoja tu.

Pamoja na changamoto hizo, Serikali kupitia MSD kila mwaka huagiza dawa hizi kwa ajili ya mahitaji hayo ya kutibu wagonjwa walioumwa na nyoka, ambapo bei ya kuinunua kutoka MSD ni TZS 200,000/= kwa kichupa kimoja. Hospitali zetu mbalimbali zimekuwa zikiagiza dawa hizi kutoka MSD na kwa washitiri wengine kwa bei hii au zaidi na kuwatibu waathirika wanaohitaji dawa za sumu za nyoka mara zinapohitajika.

Napenda kuwakumbusha kwamba kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007, huduma za tiba hutolewa bure kwa makundi maalum, au kwa kuchangiwa kwa sehemu ya gharama, au kwa kupitia mfumo wa Bima mbalimbali za Afya kama vile CHF. Kwa wale wasio na uwezo na wanaothibitishwa kuwa hawana uwezo, utaratibu wa msamaha hutumika.

Katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaohitaji dawa ya sumu ya nyoka wanahudumiwa ipasavyo, Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anatoa maelekezo yafuatayo:-


Waganga Wakuu wa Mikoa na Viongozi wa Hospitali zote nchini wahakikishe kuwa Hospitali zote za umma zinaingiza dawa hii katika dawa za dharura ili iweze kununuliwa kama dawa zingine za dharura kupitia kifungu cha fedha za dawa za dharura.

Kwa wagonjwa ambao watakuwa na Bima ya Afya, basi gharama za matibabu hayo zitalipwa kwa kupitia utaratibu huo wa Bima. Wananchi wanahimizwa kujiunga na Bima za Afya (CHF/NHIF) ili kupata unafuu wa matibabu haya na mengine. Mfano CHF - gharama ya kujiunga katika Halmashauri mbalimbali kwa kaya ni kati ya shilingi 5,000/= hadi shilingi 30,000/= kwa mwaka.

Kwa wagonjwa ambao watakuwa hawana Bima ya Afya, hao watatakiwa kuchangia gharama hiyo kwa nusu ya bei ya gharama ya dawa hizi au kwa kiwango kingine kitakachoamuliwa na Mganga Mkuu wa Serikali kadri itavyohitajika.


Hii ni kutokana na ukweli kwamba kung'atwa na nyoka ni ajali na wananchi wengi wanaopatwa na ajali hii wapo maeneo ya vijijini ambao kimsingi uwezo wao wa kumudu gharama hizi kubwa za matibabu ya dawa ya sumu ya nyoka ni mdogo.

Wagonjwa watakaothibitika kuwa hawana fedha za kuchangia gharama hiyo, basi hospitali husika kwa kupitia mpango wa msamaha wa kulipia huduma za afya wahakikishe kwamba wanampatia mgonjwa huduma hizo kwa utaratibu wa msamaha wa gharama hizo.


Aidha, kwa kuwa nchi yetu ni kubwa na ina nyoka wengi, Mhe Waziri wa Afya anawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kupitia kwa uangalifu takwimu za wagonjwa walioumwa na nyoka katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 na kuziwasilisha Wizarani kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili kupata takwimu za mahitaji halisi ya dawa ya sumu ya nyoka nchini. Hii itasaidia kuboresha upangaji, uagizaji na upatikanaji wa dawa hizo nchini.

Vile vile, Waziri wa Afya ameiagiza Bohari ya Dawa (MSD) kuweka utaratibu wa haraka wa kununua dawa hizo moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kupata unafuu wa bei.


Imetolewa na:-
Nsachris Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Afya
26/12/2016

Read More »

Serikali yapiga Marufuku Kuagiza Nyama ya Kuku Kutoka nje ya Nchi ili kulinda afya za walaji

Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.

Katazo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kupata ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.

Ole Nasha amesema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa kiwango kikubwa cha nyama.

Amewataka wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya nchi.

Ameongeza kuwa tayari serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa viongozi wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza nyama hizo za kuku wa nje nchini.

Read More »

JINSI YA KULAINISHA NYWELE ZA ASILI NA KUKUZA NYWELE ZAKO


Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair,tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo.Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia,karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.
Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi.Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani?Zina tabia gani?Zinataka nini?
1.Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.
Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi.Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako.Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri.Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

2.Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.


3.Linda unyevu wa nywele zako
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

4.Zifahamu nywele zako
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi.Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu.Unajuaje?
Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.
Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.

Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.
Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.
Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya uvuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.
Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.

5.Mafuta ya Kupaka kichwani.
Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia.Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana.Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya Zaituni Olive(extra virgin) na ya Tea tree.

6.Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.
Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako.Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana.sio kitana.Chanuo kubwa(wide toothed comb).

7.Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.
Kama unataka zikue haraka,usizisumbue sana.Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu.Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo.Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka.Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.

8.Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi.Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24.

Read More »

Nafasi 594 za Kazi Kiwanda Cha Dangote ,Jinsi ya kuomba kazi soma hapa

NAFASI ZA KAZI DANGOTE CEMENT KUMBU NO;DIL/A00/2016/01

Kiwanda cha kuzalisha saruji cha DANGOTE Tanzania kilichopo mkoani Mtwara kilomita 23 barabara ya Lindi, Kata ya Mayanga, Kijiji cha HIARI, kinaalika maombi ya nafasi za kazi za madereva wenye uzoefu wa magari makubwa ya mizigo yasio pungua uzito wa tani 33 na urefu usiopungua mita 18


DEREVA GARI ZA MIZIGO NAFASI 594

SIFA ZA MWOMBAJI

I. Awe na umri wa miaka 26 hadi 55

II. Awe na lesini halali ya daraja E na mwenye uzoefu usiopungua miaka mi 5 ya kuendesha magari makubwa ya mizigo uzoefu wa kuendesha maroli wenye urefu usiopungua mita 18

III. Uzoefu usiopungua miaka mi 5 kwenye magari ya kuvuta tela

IV. Ajue kuandika taarifa na uzoefu wa kuweka kumbu kumbu zake kwa ufasaha

V. Awe na afya njema, akili timamu, ari ya kufanya kazi kwa tija, mwadilifu, mbunifu awezaye kujisimamia mwenyewe, katika kutimiza majukumu atakayo pewa

VI. Awe na wadhamini wanaoaminika na awe tayari kuchukuliwa alama za vidole

VII. Awe na uelewa wa kusoma na kuandika na kusikia Kiswahili na kingereza kwa uufasaha muhitimu wa kidato cha IV/VI

VIII. Awe mtumiaji mzuri wa muda katika safari atakazo pangiwa ndani na nje ya nchi

IX. Awe na uwezo mzuri wa kupaki garikwene nafasi zinazo bana

X. Awe na uwezo wa kusoma kiongoza ramani


VIAMBATANISHO

- Barua ya maombi ichapishwe au iandikwe kwa mkono

- Picha 2 za rangi zilizobanwa na vizuri katka barua ya maombi

- Vyeti vya mafunzo VETA/NIT pamoja na taaluma

- Cheti au barua kutoka muajiri wa sasa au aliyepita

- Barua toka kwa wadhamini wa 2 wanaoaminika zikiambatana na picha zao

- Cheti cha afya kutoka hospitali inayotambulika na serikali

- Cheti za kuzaliwa

MSHAHARA KWA MWEZI

DILSS Faraja lla 2 ngazi ya 3


NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI

- Andika nafasi unayoomba upande wa juu kulia mwa bahasha sambamba na kumbu kumbu namba ya tangazo

- Pamoja na maelezo ya uombaji onyoesha chanzo cha taarifa ya uombaji

- Maombi yatumwe kwa njia ya posta kupitia anuani zilizopo hapo chini

- Barua za mkononi hazitapokelewa

- Barua zote zitumwe kwa

MKUU WA IDARA YA RASILIMALI WATU NA UTAWALA,

DANGOTE INDUSTRIES LIMITED TANZANIA,

S.L.P 1241,

MTWARA

Read More »

Utafiti wa NIMR Wagundua watu 83 waliougua ugonjwa wa zika Hapa Nchini Tanzania

Watu 83 hapa chini wamegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa zika kati ya watu 533 waliochukuliwa sampuli za damu.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Bugando, umeonyesha kuwa watu hao walipata maambukizi hayo kati ya mwaka 2015 na 2016.

Wakati NIMR ikitoa ripoti yake ya utafiti kuhusu kugundulika watu waliokuwa na virusi vya zika nchini, Januari 31 Serikali ilitoa taarifa kukanusha kuwapo kwa ugonjwa huo nchini.

Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitaarifu: “Kumekuwepo na taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhusu Homa ya Zika ambao ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kijulikanacho kama “Zika Virus”.

“Ugonjwa wa Homa ya Zika bado haujaingia Tanzania. Wananchi waondoe hofu juu ya uwepo wa ugonjwa huu. Hata hivyo, ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya zika, dengue na malaria ambayo huenezwa kwa namna inayofanana.”

Jana, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Mwele Malecela alikutana na waandishi wa habari kueleza ripoti ya utafiti wao ikionyesha zika ipo Tanzania na wanaendelea na utafiti kujua ukubwa wa tatizo.

“Utafiti huu ulifanyika kuanzia mwaka 2015 hadi 2016 katika mikoa nane, ambapo jumla ya sampuli 533 za damu zilipimwa na kati yao, watoto wachanga 80 walizaliwa na ulemavu wa viungo mbalimbali ambapo baada ya kufanya utafiti tulibaini asilimia 43.8 ya watoto hao wachanga walikuwa wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa zika katika mikoa hiyo,” alisema Dk Malecela.

Aliitaja mikoa iliyofanyiwa utafiti huo kuwa ni Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Kigoma, Tabora, Singida na Morogoro na kwamba bado taasisi hiyo na Chuo Kikuu cha Bugando wanaendelea na utafiti huo ili kujua ukubwa wa tatizo hilo katika mikoa hiyo.

Dk Malecela alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo alisema kati ya watu 533 waliopimwa, watu 83 sawa na asilimia 15.6 waligundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa zika na hivyo kupatiwa matibabu ya haraka.

“Kwa wale watoto wachanga 80 waliozaliwa na ulemavu, asilimia 43.8 walikuwa wameambukizwa virusi vya zika na mpaka sasa bado tunaendelea na utafiti kubaini ukubwa wa tatizo hili na kuchukua hatua za haraka,” alisema Dk Malecela.

Alisema kwa sasa wanaendelea na utafiti katika mikoa hiyo kwa wanawake waliopata matatizo ya kuharibika kwa mimba ili kujua ukubwa wa tatizo hilo.
Dk Salvatory Florence kutoka Idara ya Magonjwa ya Watoto ya Hospitali ya Hubert Kairuki alisema ugonjwa huo hauna tiba ni kama ugonjwa wa dengue ulivyo ambapo mgonjwa anapaswa kunywa maji mengi.

Dk Florence ambaye pia ni Mhadhiri Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, alisema wajawazito wa miezi mitatu wapo katika hatari ya kuzaa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na watoto wenye vichwa vidogo (microcephalus) endapo wataambukizwa virusi hivyo kupitia kwa mama zao.

“Zika ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kijulikanacho kama “Zika Virus na unaenezwa na mbu aina ya Aedes ambaye huwa ana tabia ya kuuma asubuhi na pia nyakati za mchana na wakati mwingine jioni,”alisema Dk Florence.

Pia, utafiti wa Nimr ulionyesha kuwa waendesha bodaboda katika mkoa wa Dar es Salaam, wapo hatarini kupata virusi vya Ukimwi.

Utafiti huo uliofanyika katika jiji hilo Agosti mwaka huu, umeonyesha kuwa licha ya madereva hao wa pikipiki kuwa na maambukizi madogo ya VVU kwa asilimia 2.5, bado wapo hatarini kutokana na kuwa na wapenzi wengi huku wengi wao wakigoma kutumia kinga.

Read More »

Jinsi ya kupunguza unene haraka


Ukizungumza na watu wengi wanene wanataka kujua njia ya kupunguza mafuta tumboni. Njia rahisi na salama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kitambi ni ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.

Kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi.

Vyakula kama viazi mviringo, wali, mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu unasababisha kuongezeka uzito na pia huongeza ukubwa wa tumbo.

Vyakula hivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi kidogo sana. Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko kawaida hali hiyo inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi, kutokunywa maji ya kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum.
Vyakula vya wanga na mafuta hufanya mtu kunenepa, acha au kupunguza kula vyakula hivyo.

Tumbo kuwa kubwa ni dalili kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya mwili.

Kwa kuwa chakula hiki cha ziada huwa hakitakiwi, mwili hukibadilisha na kuweka akiba katika mfumo wa mafuta kitaalam kama glycogem.

Unaweza kukabiliana na kuzidi kwa protini zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba kwa mfumo huo wa mafuta. Mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia mlo wake kwa siku kama ifuatavyo.

Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika hali inayotakiwa.

Watu wengi wanatumia chakula cha wanga mwingi wakati wa usiku, muda ambao wanakwenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa tumboni na kwenye makalio.

Mazoezi ya viungo husaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili. Wanaume huwa na asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na wanawake ni asilimia 13 hadi 25.

Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni katika mapafu na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili. Kwa ushauri zaidi wasiliana na daktari.

Read More »

Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu na afya


Katika ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.

Leo nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magonjwa.

KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.

TUFAHA, TANGO NA FIGILI

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu (cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.

NYANYA, KAROTI NA TUFAHA

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.

TANGO CHUNGU,

TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.

CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.

NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.

TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI'
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu'.

PEASI NA NDIZI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juisi yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.

PAPAI, NANASI NA MAZIWA
Juisi hii ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.

NDIZI, NANASI NA MAZIWA

Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.

Ili kupata faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake. Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri na uyatayarishe kwa kuzingatia kanuni ya ‘mtu ni afya'.

Unaweza kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.

Read More »

FAIDA ZA PARACHICHI KUANZIA JUISI YAKE MAJANI NA TUNDA LENYEWE



Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.

VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.

Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .

FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.

Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.

HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.

Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.

Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.

Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.
Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.

Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee...

 Faida Nyingine  ni pamoja na :
i. Avocado lina vitamini A,B na C ambazo zina faida lukuki kwa mwili wa mwanadamu
ii. Husaidia kuimarisha guvu ya mwili na ubongo
iii. Husaidia kujenga neva na fahamu
iv. Husaidia kujenga mifupa na kuipa nguvu
v. Husaidia kuleta kuona vizuri
vi. Husaidia kupiga vita ukosefu wa damu (anaemia)
vii. Husaidia kufanya kazi ya kuondoa nywele zinazoanguka.
viii. Husaidia kukuza nywele zinazodumaa (dandruf)
ix. Husaidia kutuliza maumivu pindi inapopakwa au kusuguliwa sehemu yenye maumivu


x. Majani ya avocado yakichemshwa kama chai na kunywewa husaidia kuondoa matatizo mbalimbali ya mwili kama vile uchovu,udhaifu,kujisikia ovyo,kuumwa kichwa, kuumwa Koo (throat),tumbo Mapafu,uvimbe, vidonda mdomoni (kwa kutafuna majani)

Mbegu ya parachichi iliyo kaangwa na kusagwa husaidia kutibu tatizo la Kukwama kwa mkojo


JINSI YA KUTUMIA PARACHICHI KAMA DAWA YA KUTIBU TATIZO LA KUKWAMA KWA MKOJO.

Koroga vijiko 2 vya chai vya unga wa mbegu ya parachichi katika maji ya moto kikombe kimoja.


MATUMIZI
Tumia kunywa kikombe kimoja mara mbili kwa siku asubuhi na jioni hadi pale tatizo lako litakapo malizika.


xi. Tunda la parachichi husaidia kutoa uric acidmwilini inayo sababishwa na ulaji wa nyama nyekundu.

Read More »

Matumizi na faida za asali katika afya ya binadamu


ASALI inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na mdalasini.

Aidha, uchunguzi wa kila wiki unaofanywa na jarida la World News kuhusu tiba unasema, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea,imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na
mdalasini katika kujenga afya bora.

Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork.

Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwamba matumizi ya kila siku ya asali yanapunguza viwango vya lehemu mwilini.

Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha imegundulika na wataalamu kwamba hupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti mmoja wa Hispania imethibitisha kwamba, aina ya dawa moja asilia iliyofanikiwa kuharibu vimelea viletavyo mafua ilitengenezwa kwa kiwango kikubwa na asali.

Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo. Asali inaaminika pia huamsha hamu ya tendo la ndoa. Wale ambao mambo katika eneo hilo si mazuri wanashauriwa angalau kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Kuna wakati asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya kuwaongezea mihemko.

Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji, itapunguza hali hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

Utamaduni wa kula asali pamoja na mdalasini, huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi uliofanywa huko India na Japani kwa miaka mingi. Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia, mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara wakati wa kifungua kinywa.

Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku nyuzi nyuzi zake ni muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa waliofanyiwa utafiti. Shinikizo la damu, pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali iliyochanganywa na mdalasini.

Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja, wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba unaonesha kwamba, asali ina hazina kubwa ya virutubisho na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga, itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea virusi na bakteria. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia pia. Inasemekana kuwa, unaweza kuishi hadi miaka 100 ukifurahia maisha ya afya bora na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai iliyowekwa mdalasini na asali.

Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10, kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne, watafiti wanasema.

Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo watafiti wanasema changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi.

Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee. Asali, wanasema inairudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu waharibifu kama dondola, washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

Utafiti uliofanywa karibuni nchini Australia na Japan, umeonesha kuwa, asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa ya kutibu saratani. Katika utafiti uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wakitumia madawa ya saratani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi," anasema Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya kwamba, sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.

Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9:00 alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka," anashauri Dk Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.

Asali inao uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

Baadhi ya watu Marekani ya Kusini, wanasukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi ili kufanya harufu mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya Kusini Mashariki, watu hutumia kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis).

Wataalamu wanaamini kwamba, uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni. Dozi za kila siku za asali na mdalasini, hufanya hali ya usikivu murua kwa wanafunzi wawapo darasani au viongozi mkutanoni kama ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani. Hiyo ndiyo asali. Ni chakula na dawa. Lakini inayozungumzwa hapa ni asali mbichi ambayo inapatikana kwa wingi Tanzania, lakini tatizo kubwa ipo pia feki inayouzwa kama mbichi!

Kwa hisani ya AFYA.KWANZA

=============

Toafauti ya asali ya nyuki wadogo na nyuki wakubwa


Asali za NYUKI WAKUBWA na WADOGO zina tofautiana katika mambo kadhaa na hvyo ni muhimu kujua tofauti hizo kabla hujanunua ili kua na uhakika.​


NYUKI WADOGO
1. Ni nyepesi zaidi kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 24​
2. Ina ladha ya UCHACHU ingawa ni tamu sana.
3. Mara nyingi ina rangi ya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoenda kwenye WEUSI


NYUKI WAKUBWA
1. Ni nzito kuliko ya nyuki wadogo kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 17 hadi 20.
2. Ni tamu moja kwa moja bila kua na ladha ya uchachu kama nyuki wadogo
3. Ina rangi nyingi kuanzia NYEUPE, NYANO, KAHAWIA ILIYOPOA, KAHAWIA ILIYOKOZA n.k


Hizo ni tofauti za muhimu kuzijua kwani zitakuwezesha kupata asali unayoitaka na kuepuka usumbufu.

Read More »

Utafiti Kumnyonya mwanamke maziwa kunasaidia kupunguza ugonjwa wa kansa ya maziwa


Kutokana na report ya mtandao wa BBC madaktari wanasema wanawake wanapunguza uwezekano wa kupata kansa ya matiti kwa kunyonywa sana matiti yao na kwa nguvu.

Kunyonywa Matiti kunapunguza hatari ambayo hutengeneza uvimbe ambao husababisha kansa ya matiti.

Matiti yanatakiwa yanyonywe mara kwa mara kwa kadri iwezekanvyo. Wasaidie wanawake zenu kupambana na kansa ya matiti.


Funny but true, a BBC report has suggested that
men and women should have their breasts sucked
thoroughly, to help them stay away from breast
cancer.
The BBC report suggested that breast sucking by
men and women can reduce the risk of developing
breast cancer for both sexes. The report published by
the BBC indicates that breast sucking has the
tendency of reducing the incidence of breast cancer
in men and women who engage in the practice. Most
men find pleasure in sucking women's Tips and in
some cases; women also suck men's Tips during
love making.
Breast cancer is the most common cancer diagnosis
among black women, and among women worldwide.
Studies have shown that when black women follow
the same preventive measures as white women, their
death rates from breast cancer are very similar.
Although black women are less likely than white
women to develop breast cancer, they are more likely
to die from it.
It is said that thousands of women might be spared
the agony of breast cancer if they extended the
period for which they suckle their babies. A study
carried out by a group of researchers in the UK also
indicated there is a relationship between
breastfeeding and a lower risk of cancer, however
there’s still more room for further research to clearly
establish a causal link.
Breastfeeding (baby) and breast sucking (men) are
two different things
According to James Klosky (UK researcher),
“Breastfeeding, in addition to diet and exercise,
avoiding tobacco use, and engaging in safe sexual
behaviour, is one more behaviour that can potentially
ameliorate adverse late effects of cancer treatment”
Breastfeeding has been found to provide a measure
of protection against uterine, cervical and ovarian
cancers as well as breast cancer. A study by Yale
University researchers showed that women who
breastfed for two years or longer reduced their risk of
breast cancer by 50 percent.
Breastfeeding is what has been shown to reduce the
risk of breast cancer, over the years. The researchers
compared the rate at which women breastfeed
babies back in the days to present days; the rate has
reduced over the years. Women are encouraged to
breastfeed their babies longer now because it is good
for the baby's health and also good for them
(women).
Research and studies are yet to ascertain whether
breast sucking, on the other hand, also reduces the
risk of developing breast cancer but based on the
BBC report in question, doctors also recommend that
women can reduce the risk of breast cancer by
having their breasts sucked. The report indicated
that regular sucking of the breast lowers the risk
level. However, the report also indicated that the
breasts must be sucked as often as possible, to help
women fight breast cancer. In other words, a
woman’s partner needs to do his own part too by
sucking her breast as often as possible. Doctors in
the report recommend that women reduce the risk of
breast cancer by having their breasts sucked but
only regular sucking of the breast lowers the risk
level.

Read More »

FAIDA NA UMUHIMU WA KUNYWA MAJI MENGI KILA SIKU, JE UNATAKA KUBORESHA AFYA YA NGOZI.


Kunywa maji safi na salama kwa kiasi kinachostahili kiafya kunaweza kuyaboresha maisha yako na kukufanya ujihisi mwenye afya na furaha zaidi.
Kunywa maji ya kutosha kuna faida nyingi. Tukichukulia kunywa maji ya kutosha ni mithili biashara kati ya wewe na afya yako, biashara hii inalipa. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji ya kutosha .

1.Kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
Vimengenya na Kemikali mbalimbali zinazohusika na mmen’genyo au usagaji wa chakula mwilini ziko katika hali ya mchanganyiko na maji.
Ili hivi viweze kufanya kazi vizuri inatakiwa kuwe na uwiano sahihi kati yake na maji.Pia maji yanahusika katika kulainisha baadhi ya vyakula.
Pia kunywa maji ya kutosha kunaongeza ufanisi wa mwili katika kusharabu chakula.

2.Dawa ya maumivu ya kichwa.
Mara nyingine maumivu ya kichwa yanasababishwa na upungufu wa maji mwilini. Hii inamaanisha, kama una maumivu ya kichwa yanayosababishwa na upungufu wa maji mwilini unaweza kughairi kumeza vidonge vya
kutuliza maumivu na kunywa maji. Hii inawezekana kwenye baadhi ya maumivu ya mgongo pia.

3.Kuboresha afya ya ngozi.

Pendezesha ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha, Unaweza kuboresha sura na mguso wa ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha kwani maji yanasaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza unyevu kwenye ngozi .

4.Kusaidia akili yako.

Maji yanauweka ubongo katika hali nzuri zaidi na ya ufanisi zaidi. Kunywa maji ya kutosha kunamwezesha mtu kufikiria kwa ufanisi zaidi.

5.Kutatua tatizo la kukaukiwa haja kubwa (constipation)

Sehemu kikubwa ya haja kubwa ni maji. Kunywa maji ya kutosha kunaweza kukusaidia kupata haja kubwa kiulaini na mara kwa nyingi zaidi.

6.Kuboresha hali ya viungo na misuli
Maji ya kutosha yanasaidia kupunguza tatizo la kubanwa misuli na pia hupunguza msuguano katika viungo vyako.

7.Kuondoa uchovu

Maji yanachochea shughuli za kimetaboliki mwilini na kuongeza ufanisi wa ubongo kwa hiyo yanapunguza uchovu.

8.Kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa.

Uwezekano wa kupata mafua,mawe ya figo,matatizo ya ini,baadhi ya saratani n.k, unaweza kupunguzwa kwa kunywa maji ya kutosha .
9.Maji yanaweza kusaidia katika kupunguza uzito.
Kama uko katika mkakati wa kupunguza uzito maji yanaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa. Maji huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki mwilini. Ongezeko hilo la kimetaboliki husababisha mwili kutumia nishati nyingi zaidi na hivyo huweza kupunguza kiasi cha nishati ambacho kitahifadhiwa mwilini katika hali ya mafuta au kupunguza kiasi cha nishati kilichohifadhiwa mwilini.Pia ongezeko la ufanisi wa figo na ini kutokana na kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa mazao ya mafuta ya ziada mwilini.
Maji hayaongezi nishati mwilini, kwa hiyo unywapo maji badala ya juisi,soda au vyakula au vinywaji vingine ambavyo huongeza nishati au mafuta mwilini unaongeza uwezekano wa kupungua uzito.

10.Maji ni kiburudisho

Kunywa maji ya kutosha kutakufanya ujisikie vizuri na pia kunaweza kupunguza safari za hospitali. Kunywa maji ya kutosha, fanya siku yako iwe poa zaidi.
Zingatia sana matumizi ya maji hasa kwa wakati huu wa joto kali ili kuepukana na matatizo yasiyo ya lazima.

Read More »

ZIJUE FAIDA ZA PAPAI KATIKA TIBA

Dunia imejaa mimea mbalimbali ambayo yote ni kwa ajili ya matumizi yetu sisi wanadamu.

Mimea na matunda imekuwa ikitumika na wazee wetu kama dawa, hii ni kwa sababu vizazi vilivyopita kwa maana ya babu na bibi zetu hawakuwahi kuwa na hospitali wala zahanati kwa ajili ya kupata tiba, isipokuwa walikuwa wakitumia mimea kwa ajili ya chakula na tiba.

Kuna mimea mbalimbali pamoja na matunda ambayo tumezoea kuitumia bila hata kujua umuhimu wake kiafya. Ni dhahiri kuwa baadhi ya mimea huweza kutumika kama tiba katika miili yetu, tena tiba salama kabisa zisizo hata na chembe ya kemikali ambazo huwa na madhara kwa afya zetu.

Kutokana na suala hili leo kuptia tovuti hii tutakwenda kufahamu namna mmea wa mpapai unavyoweza kuwa tiba nzuri kwako ikiwa ni kuanzia kuanzia mizizi, shina, majani na hata matunda yake pia.


Asili ya mpapai ni Amerika ya kati, ambapo kuanzia matunda, majani na utomvu wa mmea huu huweza kutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali duniani. Vile vile, matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.

Inaelezwa kuwapo na utafiti zilizowahi kufanyika na kuchapishwa katika jarida lijulikanalo kwa jina la ‘Archieve’ la nchini India mnamo Oktoba 27 mwaka 2010, ambapo jarida hilo lilieleza kwamba juisi ya majani ya mpapai iliweza kusaidia wagonjwa watano waliowahi kupata homa ya dengue.

Mbali na utafiti huo, pia kuna tafiti zilizowahi kufanywa na madaktari wa nchini Marekani na Japani na kubaini kuwa, juisi ya majani ya mpapai ina uwezo wa kutibu malaria na saratani, japokuwa tafiti hizo hazikukubawaliwa kisayansi.

Aidha, wataalam wa lishe nao wanaeleza kwamba, watu wenye matatizo ya kupatwa na majipu, uvimbe na vidonda mara kwa mara huwa na upungufu wa virutubisho muhimu, ambavyo huweza kupatikana ndani ya papai, hivyo imegundulika watu wenye matatizo hayo wakitumia papai hupata nafuu na kupona haraka.

Pia papai husaidia kuleta nuru ya macho, kama inavyoaminika kwa karoti, hali kadhalika papai pia husaidia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
Hivyo wavutaji wa sigara ni vyema wakatumia tunda hili mara kwa mara ili kujipunguzia madhara ya moshi wa sigara, ingawaje ni vyema wakakumbuka matumizi ya sigara si mazuri kwa afya hivyo ikibidi ni vizuri kuacha kabisa.

Ni wazi kuwa papai ni tunda lililosheheni kila aina ya utajiri wa vitamin kuliko matunda mengine, kwani lina vitamin A, B, C, D na E.

Wataalam wa tiba za asilia pia wanaeleza kwamba tunda hili linauwezo wa kutibu tatizo la usagaji wa chakula tumboni pia hutibu kisukari na pumu na mara nyingine hata kifua kikuu.

Sambamba na hayo, wataalam pia wanaeleza kwamba utomvu wa mmea wa mpapai hutibu magonjwa ya ngozi kama vile ukurutu, mapunye na hata majeraha ya moto, kiungulia na vidonda pia.

Mbali na hayo, imeelezwa kuwa mbegu za tunda la papai hutibu ini, huku majani yake yakisaidia kutibu shinikizo la damu na hata mbegu zake pia hutibu homa.
Hali kadhalika mizizi ya mmea wa mpapai husaidia kuzuia kutapika, lakini pia papai linaweza kutumika kama kilainisho cha nyama ili iweze kuiva vizuri, hususani nyama ya ng’ombe.

Kwa kutambua baadhi ya faida hizo za mpapai sasa ni vizuri ukaanza kutumia rasilimali hii ya mimea na matunda tuliyotunukiwa na Mola wetu, ili kujiepusha na madhara yatokanayo na maradhi mbalimbali.

Read More »

Ufahamu ugonjwa wa Mba na Tiba yake


Dawa ya kutibu Maradhi ya ugonjwa wa ngozi uchukuwe tango ulioshe vizuri kisha utengeneze juisi ya matango juisi hiyo uitengeneze lakini bila kumenya maganda ya matango na uwe unakunywa asubuhi kikombe kimoja mchana kikombe kimoja na jioni na pia uendelee kutafuna matango bila ya kumenya kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu ugonjwa wako utapona.

Tiba ya mba kwa kutumia mbegu za papai

Mbegu za papai tiba ya mba
Pia mapapai yaliyoiva yanatibu mapunye (ringworm), mabichi yanatibu msukumo mkuu wa damu (high blood pressure), mapapai yanatumika kama mkuyati (aphrodisiac), yanatumika kama kituliza maumivu (analgesic), mbegu za mapapai zinapunguza maumivu ya tumbo (stomachache)

Mba au mabaka mabaka kwenye ngozi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha ngozi kukosa muonekano mzuri na hata kumfanya mhusika mwenye matatizo kujikuta akijikuna kila wakati.

Kitaalamu mba ni aina mojawapo ya magonjwa yanayoambukizwa na fangasi ambao husababisha muwasho.

Wanawake wengi wanakumbana na matatizo haya ya mba, kutokana na kupaka aina ya vipodozi vinavyowaletea athari katika ngozi zao.

Unapokumbana na tatizo la namna hii ni vizuri kujipaka dawa zinazofaa badala ya kutafuta krimu ambazo ni hatari zaidi. Mbegu za papai ni tiba nzuri na ya asili ambayo haiwezi kukuletea madhara zaidi.

Jinsi ya kuondoa mba kwenye ngozi ya uso

Mbegu za papai ni dawa ya asili inayoweza kutibu ngozi yako na kukuondolea tatizo la kuwashwa au mabaka yanayokukabili.

Namna ya Kutumia kama ni Dawa Mbegu za Papai.
Unachotakiwa kufanya ni kuzipondaponda na kujipaka kwenye eneo lililoathirika na mba. Hii itasaidia kuondoa ugonjwa huo na kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye afya nzuri.

Unaweza kutumia krimu maalum za kuondoa mba hizo, zinapatikana katika maduka ya dawa, lakini unachopaswa kufanya ni kufuata masharti na kupaka kwa umakini kwenye sehemu ilioathirika.

Waweza pia kutumia sabuni maalum ya maji, shampoo, poda na hata baadhi ya losheni zote hizi zinaweza kuisafisha ngozi yako na kuifanya iondokane na muwasho unaokukera na wakati huo kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye kuvutia.

Kitunguu swaumu pia ni dawa ya fangasi
Nunua kitunguu swaumu.Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.

Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika)

Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU 1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!!

Pia kama una presha ya kushuka usitumie hii dawa maana huwa inashusha sana presha,labda unywe na kahawa baada ya kuinywa dawa hii ili kuipandisha tena presha!

Read More »

Fahamu Mengi kuhusu Ugonjwa wa Malaria



Malaria ni nini?
Malaria ni ugonjwa wa kuambukizana unaoletwa na chembe chembe zinazoitwa plasmodium.Chembe chembe hizi huingia ndani ya mwili wa binadamu baada ya kuumwa na mbu wa kike kwa jina Anopheles. Mbu mwenye chembe chembe za plasmodium anapomuuma mtu,humuingizia baadhi ya mate yenye viini vya kuambukizana kwenye kidonda hivyo kusabaza Malaria. Viini hivi husafiri hadi kwenye maini ambapo hukaa hadi vifikie ukomavu. Viini hivi baadaye huingia na mtu kama huyu akiumwa na mbu,mbu huyu hubeba chembe chembe hizi na anaweza kumuambukiza mtu atakaye muuma.

Kuna aina 4 za Malaria: P. vivax, P. malariae, P. ovale na P. falciparum. Zimepewa majina kulingana na aina ya plasmodium inayozisababisha. Aina 3 za kwanza sio hatari lakini Falciparumni hatari sana na hata inaweza kusababisha kifo. Hii ni kwa sababu ikishaingia tu mwilini huzaana kwa wingi ndani ya damu.. Hii ni kwa sababu chembe chembe nyekundu za damu(ambazo husambaza oksijeni mwilini)zilizoadhirika huwa nzito na haziwezi kuingia kwenye kapilari. Hii husababisha kufa kwa sehemu ya ubongo,maini,mapafu,figo na matumbo kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni. Hali hii inaweza kusababisha kifo kama haita tibiwa haraka.

Malaria hutambulika vipi?


Baridi,kuuma kwa misuli na kichwa zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengi mengine. Njia ya pekee unayoweza kudhihirisha kama una Malaria ni kuenda hiospitalini kupimwa damu. Watu wengi wanaotoka sehemu zilizoadhirika na Malaria pindi wanapoona dalili hizi huenda kwenye maduka ya kuuza madawa kununua dawa za kupambana na Malaria. Huu sio ushauri mzuri. Ni muhimu kupimwa damu ili aina ya plasmodium inayosababisha maradhi yako itambulike na upewe matibabu yanayostahili.

Nani yuko kwenye hatari ya kuambukizwa Malaria?


Watoto wachanga,watoto na akina mama waja wazito wako kwenye hatarikubwa ya kushambuliwa hata kufa kutokana na Malaria. Watoto wachanga na watoto wako kwenye hatari kwa sababu wameambukizwa mara chache nahawajajenga

kinga dhidi ya chembechembe hiziVamizi la Malaria kwa wanawake wajawazito kalikwa sababu kinga yao dhidi ya maradhi huwa chini wakati wa uja uzito. Malaria huongeza tishio kwa mtoto ambaye hajazaliwa kama kuzaliwa kabla ya wakati

kutimia, uaviaji wa mimba, maambukizi ya sehemu za siri, uzani mdogo wa mtoto anapozaliwa, kupoteza uja uzito na pia ugonjwa huu unaweza kumsababishia mama kifo.


Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?



Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila kuharibu maji.
Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa


Ni zipi dalili za Malaria?


Dalili za Malaria ni kama zile za Flu; homa, baridi na kuuma kwa misuli na kichwa. Watu wengine hupatwa na kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Vipindi vya baridi, homa na kutokwa na jasho hujirudia kila siku moja, mbili au tatu. Watu wenye aina ya P. falciparumwanaweza kupata Malaria ya ubongo ambayo husababisha kuishiwa na fahamu ama kuchanganyikiwa kiakili.

Tiba ya Malaria

Tiba ya Malaria inategemea mambo kadhaa:

Hali ya mgonjwa (mtoto, mama mja mzito, mtu mzima, ni kali ama sio kali)
Nguvu ya dawa dhidi ya ambukizo la viini vya plasmodium.
Eneo la kijiografia ambalo mtu aliambukizwa. Kwa mfano, P.falciparuminayopatikana katika nchi za Mashariki ya kati inaweza kutibiwa na dawa ya chloroquine, lakini inayopatikana Africa, katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara haitibiki kwachloroquine.
Aina ya plasmodium inayodhuru mgonjwa. Malaria yasiyo makali hutibiwa na dawa za kumeza ilhali wagonjwa wenye P. falciparum kali hulazwa hospitalini na kupewa sindano ya maji.

Read More »

Hatua Kuu za Ugonjwa wa VVU/UKIMWI (HIV/AIDS stages) na Dalili Zake



Ugonjwa wa HIV/AIDS umekuwa janga kubwa sana duniani kwa sasa kutokana kuathiri watu wengi na kukosekana kwa tiba ya ugonjwa huu. Maambukizi ya ugonjwa wa HIV/AIDS hufahamika kama maambukizi ya VVU (Virusi vya Ukimwi). Mtu anapopata magonjwa nyemelezi (opportunistic infections) ndiyo huwa tunasema mtu amepata ugonjwa wa UKIMWI au AIDS.


Je ni kuna hatua ngapi za ugonjwa wa VVU/UKIMWI na dalili zake ni zipi?
Kwa mujibu wa uanishaji uliofanywa na wataalamu wa shirika la Afya Duniani yaani WHO, kuna hatua (stages) kuu nne za ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambazo ni:

1. Hatua ya kwanza [Primary HIV Infection]

Hatua hii huwa kwa muda wa wiki nne. Ni asilimia 20 tu ya watu wenye maambukizi ya VVU walio kwenye hatua hii ambao hupata dalili na viashiria vikali vya ugonjwa huu lakini mara nyingi madaktari hushindwa kutambua kama mgonjwa amepata maambukizi ya VVU kutokana na dalili na viashiria vyake hapa kufanana sana na dalili za magonjwa mengine. Mgonjwa aliye katika hatua hii ya kwanza ya maambukizi ya VVU huweza kuonesha dalili na viashiria kama vile kuvimba tezi (swollen lymph glands), kupatwa na homa kali, kuumwa koo (sore throat), kujihisi mchovu, kujihisi maumivu sehemu mbalimbali mwilini (body aches), kutokwa na vipele mwilini (skin rash), na pia kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo

Mgonjwa anayepata dalili na viashiria hivi tunasema kwamba amepata “Acute HIV infection/Acute HIV retroviral infection au seroconversion illness.” Dalili hizi hutokana na mwili wa mtu mwenye maambukizi ya VVU kuanza kutengeneza kinga dhidhi ya VVU.

Hatua ya Pili (Clinically Asymptomatic Stage)
Katika hatua hii ambayo inaweza kudumu kwa muda wa miaka kumi, mgonjwa anakuwa haonyeshi dalili/viashiria vyovyote vile isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba [swollen lymph nodes]. Kiwango cha VVU kwenye damu hupungua sana lakini mgonjwa anaweza kuambukiza mtu mwingine yoyote na vipimo vya VVU vina uwezo wa kutambua uwepo wa maambukizi y VVU katika damu.

Tafiti mablimbali zimeonesha kwamba VVU katika mwili huwa bado zinazaliana [active] na hukimbilia/hujificha kwenye tezi [lymph nodes]. Kutokana na kujificha kwake katika hatua hii, kipimo cha kupima wingi wa virusi vya ukimwi (Viral load test) katika mwili hutumiwa sana ili kuweza kutambua uwepo wa VVU. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.

Hatua ya Tatu [Symptomatic HIV infection]
Kutokana na kuongezeka kwa wingi wa VVU katika mwili, kinga ya mwili huzidi kudhoofika na hii husababishwa na;
• Tezi na tishu zilizoathiriwa na VVU huharibika kutokana na maambukizi ya muda mrefu
• VVU hubadilika badilika na kuwa na uwezo zaidi wa kuathiri tishu na sehemu mbalimbali za mwili na hata kuziua/kuziharibu seli zinazokinga mwili kutokana na maambukizi zinazojulikana kama T helper cell
• Mwili hushindwa kumudu uharibifu wa T helper cell na kushindwa kuzalisha seli nyingine mpya.

Dawa za kuvubaisha VVU au Antiretroviral therapy huanza kutumiwa wakati seli aina ya CD4 zinapopungua na kuwa kiwango cha chini sana. Kupungua kwa seli hizi za CD4 ni kielelezo cha kinga ya mwili kuwa dhaifu. Matumizi ya dawa hizi huboresha kinga ya mwili na kumfanya mgonjwa kuishi kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili au viashiria vyovyote vile [yaani kumrudisha mgonjwa katika hatua ya pili].

Kama mgonjwa wa VVU hatumii dawa za kuvubaisha VVU au anatumia ARV's ambazo hazimsaidii au hazifanyi kazi vizuri mwilini mwake, basi mgonjwa ataendelea kuingia kwenye hatua ya nne ya Ukosefu wa Kinga Mwilini (Ukimwi) au AIDS.

Hatua ya Nne [UKIMWI]

Kama nilivyoeleza hapo juu, hatua hii hujulikana kama Ukosefu wa Kinga Mwilini [UKIMWI] au AIDS, ambapo mgonjwa hupata maambukizi ya magonjwa nyemelezi pamoja na saratani za aina mbalimbali kutokana na kupungua kwa kinga mwilini.

Vigezo vilivyopangwa na shirika la afya duniani (WHO) ili kuweza kutambua kama mgonjwa yupo kwenye hatua hii ya UKIMWI hutofautiana kati ya watu wakubwa na watoto chini ya miaka 5. Pamoja na kuwa WHO wameweka vigezo vya pamoja, utambuzi wa hatua za ugonjwa wa UKIMWI hutofautiana kati ya nchi na nchi kutokana na miongozo tofauti ya nchi hizo.

Kwa watu wazima na watoto walio na umri zaidi ya miaka mitano, uwepo wa ugonjwa wowote nyemelezi pamoja na kushuka kiwango cha CD4 chini ya 200 cells/mm3 au kushuka kwa seli za CD4 chini ya asilimia 15 hutambulika kama ugonjwa wa UKIMWI.

Kwa watoto walio chini ya miaka mitano, uwepo wa ugonjwa wowote nyemelezi/kushuka kwa seli za CD4 chini ya asilimia 20 [kwa wale wenye umri kati ya miezi 12-35] hutambulika kama wana ugonjwa wa UKIMWI.

Watoto wenye umri chini ya miezi 12, kupungua kwa seli za CD4 chini ya asilimia 25 ndiyo hutumika kutambulisha wana ugonjwa wa UKIMWI.

CD4 ni nini?
CD4 ni aina ya protini inayopatikana katika ukuta wa seli zinazojulikana kama T helper cell [pia hujulikana kama CD + lymphocyte]. VVU hushambulia na kujishikiza kwenye protini hii kabla ya kupata uwezo wa kuathiri seli za T helper cell. Seli hizi za T helper cell ndizo hulinda mwili dhidi ya maambukizi mbalimbali na hivyo kuchangia katika kustawi kwa kinga ya mwili. Kupungua kwa seli hizi mwilini husababisha kupungua kwa kinga ya mwili na hivyo mtu kupata magonjwa mbalimbali.

Magonjwa nyemelezi/saratani (opportunistic infections/cancer)
Baadhi ya magonjwa nyemelezi yanayoweza kumpata mtu mwenye ugonjwa VVU/UKIMWI ni pamoja na
a. magonjwa ya mfumo wa kupumua kama vileugonjwa wa homa ya mapafu (pneumocyctic carinii pneumonia), Kifua kikuu (TB) na Kaposi’s sarcoma (saratani);
b. Magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile Cryptosporidiosis, Candida (fangasi), Cytomegolavirus (CMV), Isosporiasis, na Kaposi's Sarcoma
c. Magonjwa ya mfumo wa fahamu (Central/peripheral nervous system) kama vile Cytomegolavirus, Toxoplasmosis, Cryptococcosis, Non Hodgkin's lymphoma (saratani), Varicella Zoster (mkanda wa jeshi), Herpes simplex
d. Magonjwa mbalimbali ya ngozi [skin diseases] kama vile Herpes simplex, Kaposi's sarcoma (saratani ya ngozi) na Varicella Zoster [mkanda wa jeshi]

Hatua za VVU/UKIMWI kulingana na dalili za ugonjwa [clinical classification of HIV/AIDS]
Kutokana na uhaba wa vifaa vya kupimia kiwango cha seli aina ya CD4 katika nchi mbalimbali, shirika la afya duniani, limetengeza muongozo mwingine ambao utamsaidia mhudumu wa afya kuweza kutambua kama mgonjwa amefikia hatua ya ugonjwa wa UKIMWI na anastahili kuanza tiba au la. Uainishaji wa namna hii huitwa clinical classification of HIV/AIDS.



Hatua ya Kwanza [Clinical stage I]

• Mgonjwa hana dalili zozote (asymptomatic)
• Kuwepo kwa uvimbe katika tezi ambao hauondoki (persistant lymphadenopathy)




Hatua ya Pili [Cilinical stage II]
• Kupungua uzito chini ya asilimia 10 ya uzito wa mwili bila sababu maalum
• Magonjwa ya mara kwa mara kwenye mfumo wa upumuaji kama magonjwa ya masikio, kinywa, tezi la koo nk (sinusitis, tonsillitis, otitis media, pharyngitis)
• Mkanda wa jeshi (Herpes zoster)
• Vidonda pembezoni mwa mdomo (Angular chelitis)
• Vidonda vya mara kwa mara kwenye kinywa (Recurrent oral ulceration)
• Vipele mwilini (Papular pruritic eruptions)
• Ugonjwa wa ngozi [Seborrhoeic dermatitis]
• Maambukizi ya fangasi katika kucha [Fungal nail infections]

Hatua ya Tatu [Clinical stage III]

• Kupungua uzito kwa zaidi ya asilimia 10 ya uzito wa mwili bila sababu yoyote maalum
• Kuharisha zaidi ya mwezi mmoja bila sababu yoyote maalum
• Kuwa na homa isiyoelezeka [homa hii inaweza kuwa inapona na kujirudia au homa ambayo inakuwepo kwa zaidi ya mwezi mmoja]
• Maambukizi ya fangasi kwenye kinywa [Persistent oral candiadiasis]
• Oral hairy leukoplakia
• Ugonjwa wa kifua kikuu kwenye mapafu [kwenye mapafu]
• Maambukizi hatari ya vimelea vya bakteria [homa ya mapafu, ugonjwa wa uti wa mgongo, maambukizi katika mifupa na jointi, empyema, pyomyositis, bacteraemia]
• Maambukizi hatari kwenye kinywa [Acute necrotizing ulcerative stomatitis, gingivitis or periodontitis]
• Upungufu wa damu mwilini bila sababu yoyote maalum [Unexplained anaemia (below 8 g/dl), neutropenia (below 0.5 billion/l) and/or chronic thrombocytopenia (below 50 billion/l)]

Hatua ya Nne (Clinical stage IV)
• Kudhoofika mwili [HIV wasting syndrome]
• Homa kali sana ya mapafu [Pneumocystis pneumonia]
• Saratani ya shingo ya kizazi [invasive cervical cancer]
• Homa kali sana ya mapafu inayojirudia inaosababishwa na vimelea vya bakteria
• Magonjwa ya kwenye mfumo wa figo/moyo yayochangiwa na VVU [Symptomatic HIV-associated nephropathy or HIV-associated cardiomyopathy]
• Maambukizi ya fangasi katika mishipa ya kupitisha chakula mpaka kwenye mapafu na mishipa yake ya kupitisha/kusambaza hewa mwilini
• Ugonjwa wa kifua kikuu uliosambaa mwilini [disseminated mycobacteria tuberculosis]
• Maambukizi ya fangasi yaliyosambaa mwilini [histoplasmosis, coccidiomycosis]
• Saratani ya kwenye tishu za mwili [kaposis sarcoma]
• Maambukizi kwenye mishipa ya fahamu yanayosababishwa na vimelea aina ya toxoplasma gondii [Central nervous system toxoplasmosis]
• Maambukizi ya VVU kwenye ubongo na kusababisha mgonjwa kuwa kama mgonjwa wa akili [HIV encephalopathy]
• Ugonjwa wa uti wa mgongo uliosambaa mwilini [Extrapulmonary cryptococcosis including meningitis]
• Ugonjwa wa kifua kikuu uliosambaa mwilini ambao hausababishwi na vimelea aina ya mycobacteria tuberculosis [Disseminated non-tuberculous mycobacteria infection]
• Aina ya ugonjwa unaoathiri ubongo na kumfanya mgonjwa shindwe kufikiri sawasawa [Progressive multifocal leukoencephalopathy]
• Chronic cryptosporidiosis na Chronic isosporiasis
• Recurrent septicaemia [including non-typhoidal Salmonella]
• Lymphoma [cerebral or B cell non-Hodgkin]
• Atypical disseminated leishmaniasis
• Cytomegalovirus infection [retinitis or infection of other organs]
• Chronic herpes simplex infection [orolabial, genital or anorectal of more than one month’s duration or visceral at any site].

Read More »

Tatizo la Chunusi na Namna ya Kulikabili soma hapa upate maarifa za kukufanya uonekane mpya kila siku


Chunusi ni jambo la kawaida wakati wa balehe na
zinatokea kwa sababu Mvulana au msichana
anafikia hatua ya muhimu ya maisha ya kutoka
utotoni kwenda katika utu uzima.




Wakati wa
balehe, tezi za ngozi zinazozalisha mafuta
mafuta yanayolainisha ngozi hutenda kazi zake
kwa uchangamfu mkubwa na kuzalisha mafuta ya
ngozi yaitwayo ‘sebum’.


Kazi ya sebum ni kulainisha ngozi kwa msichana
na kuleta mwonekano wa kisichana unaopendeza
na kuvutia.


Sebum inapozalishwa kwa wingi
inasababisha vinyweleo katika ngozi vizibe na
kuleta tatizo la chunusi.


Chunusi zikiwa nyingi
sana zinatazamwa kama ugonjwa wa ngozi na
hili linaweza kuwa tatizo la kurithi.

Ikiwa wazazi
au ndugu walikuwa na chunusi nyingi, kuna
uwezekano mkubwa wewe pia kupata chunusi
kwa wingi.


Hofu, woga na wasiwasi pia vinaweza kuchangia
msichana kupata chunusi. Hii huwatokea
wasichana wengi wanaopata hofu wakati wa
mitihani au muda mfupi baada ya hedhi.


Licha ya
ukweli kuwa mahangaiko ya kihisia husababisha
chunusi, tatizo la chunusi pia husababisha tatizo
la mahangaiko ya kihisia kwa wasichana wengi
wanao hangaikia urembo na uzuri wa ngozi ya
usoni.


Wasichana wengi wanaopata tatizo la chunusi
hawafurahii kile wanachokiona katika kioo
wanapojipodoa, lakini ukweli ni kwamba chunusi
hazitoshi kuwa chanzo cha kumpotezea
msichana raha na furaha katika maisha yake.


Pale chunusi zinapokuwa tatizo la kihisia,
msichana hana budi kushughulikia tatizo hili kwa
namna ambayo inadumisha afya ya mwili na akili
zake.



Jinsi ya Kukabiliana na Tatizo:


1. Safisha uso kwa maji na sabuni kila siku jioni
na asubuhi.


Fanya hivyo pia unapomaliza kufanya mazoezi au
unapotokwa na jasho.

Msichana yeyote asikubali
kulala usiku bila kusafisha uso au kuoga. Hii
itasaidia kuondoa mafuta kwenye ngozi na
kupunguza bakteria wanaoshambulia na
kusababisha uvimbe wa chunusi.


2. Usikamue chunusi ambazo hazijaiva, pia
usizishikeshike ili kuepuka makovu meusi usoni
na hatari ya kupata uvimbe wa uso pamoja na
ugonjwa hatari wa ubongo (cavernous sinus
thrombosis).


Mtu akipata ugonjwa wa ubongo unaotokana na
kukamua chunusi, anaweza kupoteza maisha
kama hakupata matibabu ya haraka na ya
uhakika na katika hali kama hii mtu mwenye
imani za kishirikina anaweza kufikiri kuwa
amerogwa.


3. Msichana mwenye tatizo la chunusi imempasa
kuepuka kutumia vipodozi vyenye mafuta na
vichocheo vya steroidi hasa katika sehemu zenye
kuathiriwa na chunusi.


Nywele zisafishwe kila siku

na mitindo ya nywele inayosababisha nywele
kugusana na ngozi ya usoni au mgongo iepukwe.


4. Pata nafasi na muda wa kukaa kwenye
mwanga wa jua kila siku hasa wakati wa asubuhi
ili sehemu zenye chunusi zipate mwanga wa jua
kwa muda wa wastani.

Mwanga wa jua unasaidia
kuimarisha afya ya ngozi na kuuwa bakteria
wanaosababisha chunusi kuvimba.


Tahadhari ichukuliwe kuhusiana na jambo hili
kwani kukaa kwenye mwanga wa jua kwa muda
mrefu hasababisha ngozi kuzalisha mafuta kwa
wingi na kuongeza tatizo la chunusi.



Jambo hili
pia linaweza kusababisha saratani ya ngozi,
kuzeeka kwa ngozi mapema au ngozi kuwa na
mikunjo na kukaukiana.




5. Kula vyakula vyenye asili ya mimea, matunda,
nafaka na mboga za majani husaidia mwili
kupambana na tatizo hili.


Kunywa juisi ya karoti
glasi moja kutwa mara tatu kila baada ya saa 8
kwa kipindi cha mwezi mmoja, husaidia katika
udhibiti wa chunusi.

Unaweza pia kupaka usoni
karoti zilizopondwapondwa na kuziacha zikae
usoni kwa zaidi ya dakika 20 kila siku kabla ya
kuziondoa kwa kunawa maji.


Karoti zina vitamini
A inayosaidia ngozi ili isipate makovu meusi
yatokanayo na chunusi.


Kunywa maji mengi kila
siku na hakikisha pia unapata mapumziko na
usingizi wa kutosha kila siku.


6. Epuka matumazi ya dawa za uzazi wa mpango
zenye vichocheo vya ujinsia kama vile vidonge
na sindano.

Tumia dawa za kusafisha ngozi kama
vile ‘benzoyl peroxide cleanser, anza na 2.5%, 5%
na hatimae 10%, kusafisha sehemu zote zenye
chunusi.


Hii husaidia kupunguza bakteria wanaoshambalia
chunusi juu ya ngozi na kuifanya ngozi iwe kavu
na kupunguza mafuta katika ngozi.

Kama chunusi
zinazidi hata baada ya kutumia tiba hiyo hapo
juu, onana na daktari kwa matibabu zaidi.

Read More »