Mchungaji afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kubaka mwanaye



Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (FPCT) Tawi la Gezaulole wilayani Hai, Emanueli Mwikizu (42) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 7.
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Anold Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha Moleli amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kuzini akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu nyumbani kwake mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo ambapo hakimu anayesikiliza kesi hiyo aliharisha hadi Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa yupo rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.